Mkuu wa wilaya ya songea mkoani Ruvuma Pololeti Mgema ametoa maagizo kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira kutoa elimu kwa wananchi wa Madaba kuhusu umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji.
Mgema ametoa maagizo hayo hivi karibuni wakati alipotembelea na kukagua chanzo cha maji cha Mgombesi kilichopo kilomita tano kutoka barabara kuu ya Songea - Njombe.
Mgema amesema wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za kiuchumi karibu na vyanzo ya maji wapewe elimu kuhusu umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji na athari zake kwa viumbe hai.
Mgema amesisitiza kwakusema wananchi wote wanaofanya shuguli za kiuchumi karibu na vyanzo vya maji ni marufuku kufanya kazi hizo kwalengo la kukabiliana na changamoto za ukosefu wa maji.
“ Maagizo yangu vyanzo vya maji vilindwe”,amesema Mgema.
Amesisitiza wataalam wa RUWASA kuongeza juhudi za kukamilisha ujenzi wa mradi huo ili uweze kutoa huduma kwa wananchi kama Serikali inavyopambana kuondoa tatizo la maji katika jamii.
Mgema amesema zaidi ya wakazi 30,000 wa vijiji vya kipingu,kifagulo,Mtepa na Lituta ndio wanufaika wakuu wa huduma hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Kijiji cha Lituta na kipingu Esta Mlelwa na Godfrey Ngatunga ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha kipingu anakili kuwepo kwa tatizo la maji katika vijij hivyo lakini kwa sasa wanatoa shukrani kwa serikali kwa kuwaletea huduma ya maji
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mzingira wa Wilaya ya Songea Mathias Pangras amesma mradi umekamilika kwa asilimia 75.
Amesema mradi umejengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza walijenga chanzo na tank la lita laki mbili,na awamu ya pili wameongeza kujenga tank mbili na kazi ya usambazaji wa maji kutoka kwenye tank kwenda kwa wananchi.
Mathias amezitaja gharama ya ujenzi ni zaidi ya shilingi bilioni mbili na milioni sabini na tisa, na mradi ukikamilika utamaliza tatizo la maji katika wilaya ya Madaba.
“RUWASA maji bombani
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Songea DC
16,12,2020
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa