Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Bi. Elizabeth Gumbo akiambatana timu ya Menejimenti ya Halmashaui ya Wilaya ya Songea, wamekua na ziara ya Siku mbili kuanzia tarehe 5-6/04/2024, ya kutembelea na kukagua miradi inayosimamiwa na Halmashauri na kutoa maelekezo na maagizo kwa mafundi na kamati ya ujenzi.
Katika ziara hiyo timu ya menegiment ilikagua Miradi ya Afya ambayo ni zahanati vituo vya Afya, Elimu walikagua Shule za Msingi na Sekondari. Miongoni mwa shule ni pamoja na Shule ya Msingi Nambalapi, Mbolongo Shule ya Sekondari Jenista Mhagama, Shule ya Sekondari ya Mpitimbi na Soko la Mazao la Kimkakati lililopo kijiji cha Matomondo kata ya Mbinga Mhalule. Walikagua pia mradi wa samaki (mabwawa ya Samaki) yaliyopo Mpitimbi
Mkurugenzi alisisitiza umakini kwenye ujenzi wa mali za umma lakini pia aliwataka wasimamizi na mafundi kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia muda waliopewa ili kuhakikisha pesa walizotengewa zinatumiaka kwa wakati na lengo la Serikali linatimia.
Aidha aliwataka pia wakuu wa Divisheni na vitengo kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa kuzungukia miradi, ili kubaini changamioto ndogo ndogo ambazo zimekua zikiibuliwa pindi wageni wanapokuja. “Niwashukuru sana timu yangu ya Menejiment kwa ziara hii, nitoe wito kwenu wote kwamba zoezi hili lisiishie hapa, tuwe na utaratibu wa kukagua miradi pindi inapokua inajengwa hii itasaidia kubaini makosa ambayo yamekua yakioneshwa pindi wageni wanapokuja kupitia na kukagua moiradi.
Kwa upande wa wananchi wamepongea na kushukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa namna ambapo imekua ikiwekeza sana nguvu kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwajengea miundombinu ya kutosha kama vile Barabara madaraja shule Zahanati ambapo vyote hivi vinapelekea unafuu wa maisha kwa wananchi
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa