• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

CHUO cha CBCTC Ruvuma kuanza kutoa kozi ya waongoza watalii

Tarehe ya Kuwekwa: June 14th, 2019

CHUO cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii (CBCTC) kilichopo katika Kijiji cha Likuyu Sekamaganga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma  kimefanya mahafali ya mafunzo kwa Askari wanyamapori wa vijiji (VGS) ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu.

Akizungumza katika mahafali hayo Naibu Waziri Kanyasu amewaasa askari wahitimu kwenda kuzilinda na kuzitunza rasilimali za taifa katika maeneo yao  ili ziwe endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Kanyasu ameahidi kushughulikia changamoto zinazokikabili chuo hicho ikiwemo miundombinu chakavu na kumalizia jengo la maktaba ambalo Naibu Waziri huyo ameweka jiwe  msingi na kwamba amesema serikali itahakikisha kuwa chuo hicho kinakuwa na sifa za chuo cha kati.

Awali akizungumza kabla ya mgeni rasmi Mkuu wa  chuo cha (CBCTC) Jane Nyau amesema chuo hicho  kilichoanzishwa mwaka 1995 ni Chuo pekee cha utoaji wa mafunzo ya uhifadhi wa maliasili kwa jamii barani Afrika na kwamba hapa nchini katika vyuo vya uhifadhi ,hakuna chuo kinachotoa mafunzo yanayofanana na chuo hiki,hali hiyo ndiyo inakifanya kuwa ni  chuo cha kipekee nchini.

Amesema katika mahafali ya kozi namba 64/2019  ya Askari wanyamapori wa vijiji(VGS)  jumla ya wanachuo 20 wamehitimu  mafunzo ya Askari wanyamapori wa vijiji (VGS) kwa miezi mitatu.

Nyau amesema licha ya chuo hicho kutoa kozi  za mafunzo ya Askari wanyamapori wa vijiji(VGS) ya miezi mitatu na mafunzo ya viongozi wa serikali na Kamati za maliasili za vijiji ya mwezi mmoja,CBCTC kuanzia Julai 2019 kinatarajia kuanza kutoa kozi ya Astashahada ya Awali ya Waongoza watalii kwa muda wa mwaka mmoja.

“Kozi hii  itatolewa ili kuendana na mkakati unaoendelea wa serikali wa kukuza utalii katika Ukanda wa Kusini,mtaala wa kozi hiyo umeshakamilika na tayari umeshathibitishwa na Baraza la Usimamizi wa Vyuo vya Ufundi (NACTE)’anasema Nyau.

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAAFISA HABARI KIMEMALIZIKA KWA KUWEKA MAKUBALIANO ENDELEVU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI

    May 24, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA, WANATEGEMEA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KATIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI SONGEA

    May 21, 2025
  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa