Divisheni ya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Songea, imeanza Kampeni ya kitaifa ya Chanjo kwa siku tano kuanzia jumatatu hadi ijumaa kwa watoto wa kike dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi.
Chanjo hiyo ni mahsusi kwa ajili ya kuwakinga dhidi ya virusi vinavyoitwa (Human Papilloma Virus) HPV ambavyo vinapelekea saratani ya Mlango wa kizazi kwa wanawake.
“Waathirika zaidi wa ugonjwa huo ni wanawake na si wanaume. Chanjo hiyo inatolewa kwa watoto kati ya miaka 9 hadi 14’ Dr. Kihaule.
Mganga Mkuu wa Halmashauri Dr. Geofrey Kihaule Anatoa wito kwa wazazi wote wenye watoto umri kuanzia miaka tisa hadi kumi nne (9-14) khakikisha wanafika mashuleni au kwenye vituo vya kutolea huduma ya Afya kwa ajili ya kupata chanjo hiyo .
Chanjo hii ni bure haina malipo yeyote hivyo wazazi msisite kuleta watoto waje kuchanja. Chanjo hii haina madhara yeyote kwa binadamu ila inafaida kubwa kwani inakukinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi.
Akizungumzia juu ya upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu kuhusu chanjo hizo, Dr. Geofrey Kihaule amesema “Chanjo hizi ni salama, lengo ni kuwakinga wanawake dhidi ya Saratani ya kizazi, haina madhara yeyote, Serikali imeamua kuwachanja watoto ili kuwakinga pindi watakofikia umri wa utu uzima, hii ni kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya Wanawake walioathilika na Saratani ya Mlango wa kizazi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa