Chakaga atoa wito kwa Halmashauri za mkoa wa Ruvuma kuelimisha mabaraza ya ardhi sheria ya ardhi
Kamanda wa TAKUKURU mkoani Ruvuma Christina Chakaga ametoa wito kwa Halmashauri za mkoa wa Ruvuma kutoa elimu ya sheria kwa mabaraza ya ardhi ya Kata kwa lengo la kupunguza migogoro ya ardhi.
Chakaga ametoa wito huo wakati akitoa taaifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Aprili hadi Julai 2019 katika ofisi za TAKUKURU.
Amesema mabaraza ya ardhi ya Kata yanafanya kazi za kisheria,wakati hawana elimu ya sheria jambo linalo sababisha kuongezeka kwa vitendo vya rushwa katika idara ya ardhi wakati wa kutatuamigohoro baina ya mlalamikaji na mlalamikiwa.
Kwakipindi cha miezi mitatu TAKUKURU mkoani Ruvuma imepokea taarifa za malalamiko ya rushwa 63 toka vyanzo mbalimbali ambapo kati ya malalamiko hayo idara ya ardhi inaongoza kwa kulalamikiwa kwa malalamiko 17,ikifuatiwa na idara ya elimu yenye malalmiko 10 na ya misho kulalamikiwa ni taasisi za kifedha zenye malalamiko mawili.
Aidha taasisi imefanya ufutiliaji wa zaidi ya shilingi bilioni 14 ambazo zimetolewa na serikali kwa ujenzi wa miradi ya miundo mbinu ya ujenzi, maji,afya,elimu na barabara nakubaini dosari ndogondogo ambazo zimeshatolewa ushauri wa wanamna ya kurekebisha dosari hizo.
Akizungumzia kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika nchini, Chakaga amewataka wagombea na wapiga kura kujiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vitawasababishia matatizo ya kuchukuliwa hatua za kisheria kulingana na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 ya kuongoza vita zidi ya rushwa na ufisadi nchini.
MWISHO. 17 / 07 / 2019.
JACQUELEN CLAVERY –SONGEA DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa