• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

BRIGEDIA Jenerali Ibuge akagua mpaka wa nchi ya Tanzania na Msumbiji

Tarehe ya Kuwekwa: June 10th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amefanya ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa kwa kukagua eneo la Mkenda lililopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji kupitia Wilaya ya Songea.

Brigedia Jenerali Ibuge amekagua daraja la Mkenda Mto Ruvuma linalotenganisha nchi ya Tanzania na Msumbiji, amezungumza na askari wa Msumbiji waliopo mpakani,ametembelea kivuko cha Mitomoni,kupitia Mto Ruvuma,amekagua soko la kimataifa la Mkenda na kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Mkenda.

Akizungumza na watumishi wa Idara za uhamiaji,Mamlaka ya Mapato Tanzania,polisi na Usalama waliopo eneo la Mkenda,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amelitaja lengo la serikali kuwaweka watumishi hao mpakani ni kusimamia maslahi ya Taifa.

Amewataka watumishi hao kila mmoja katika Idara yake kushirikiana na kufanya kazi kwa tija na ufanisi kwa maslahi ya watanzania.

“Sasa hili la ushirikiano nataka kusisitiza,mpo mbele ya mpaka wetu ,kumbukeni kuna changamoto kubwa ya ugaidi inayotukabili kwenye mpaka wetu na Msumbiji ,huu sio wakati wa kuchukulia vitu poa’’,alisisitiza Brigedia Jenerali Ibuge.

Hata hivyo amewatahadharisha watumishi hao wasipokuwa na muunganiko wanapobaini watuhumiwa wakiwemo wahamiaji haramu, biashara zinazotia mashaka na vitendo vya rushwa wanaweza kuharibu mfumo mzima wa Mkoa na Taifa kwa ujumla kutokana na uzembe.

Kuhusu watumishi wa TRA waliopo mpakani,RC Ibuge amesema licha ya ukweli kuwa mapato ni muhimu kwa maendeleo ya nchi,hata hivyo ametaka ushirikiano wa kuangalia mazingira ya kiforodha yaangaliwe kiulinzi na usalama kwa kudumisha mawasiliano na vyombo vingine vya usalama.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa ametoa pole na kuwafariji wananchi wa kijiji cha Mkenda kutokana na vifo vilivyotokea katika ajali ya majini kwenye mto Ruvuma hivi karibuni.

Hata hivyo ametoa rai kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mkenda na wananchi kwa ujumla kushirikiana na vyombo vya usalama vilivyopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji ili kujilinda kwa ajili ya usalama wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Awali akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Kituo cha Uhamiaji Mkenda,Mratibu Msaidizi wa Uhamiaji Upendo Kikudo amesema kituo hicho kinafanya kazi kwa ushirkiano na Idara nne ambazo ni Uhamiaji,Polisi,TRA na Usalama wa Taifa.

Amezitaja changamoto zinazokikabili kituo hicho ni ukubwa wa mpaka kutokana na jiografia ya eneo lililozungukwa na Mto Ruvuma na misitu,hali ya machafuko inayoendelea nchini Msumbiji,uwepo wa vipenyo vingi vilivyo rasmi na visivyo rasmi,mawasiliano,miundombinu ya barabara,huduma za afya na ukosefu wa nishati ya umeme.

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAAFISA HABARI KIMEMALIZIKA KWA KUWEKA MAKUBALIANO ENDELEVU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI

    May 24, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA, WANATEGEMEA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KATIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI SONGEA

    May 21, 2025
  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa