Bilioni mbili Milioni mia tano thelathini na tano (2,535,000,000) Zimeijenga Shule ya Sekondari Jenista Mhagama iliyopo kata ya Parangu, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma
Shule hiyo yenye jina la Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambeye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu) ilijengwa mwaka 2020 na inajumla ya majengo 126.
Akizungumza kwa niaba ya Shule hiyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Jenista Mhagama Mwl. Felista Lwambano alisema “ Shule yetu ilianza mwaka 2020, kwa sasa ina jumla ya majengo 126, ambayo ni Madarasa 34, Maabara 4, Nyumba za Walimu 8, Maktaba 1, jingo la Tehama 1, Jengo la Utawala 1, Bwalo 1 na vyoo matundu 67.
Shule ya Jenista Mhagama inauwezo wa kuchukua wanafunzi 1360, ila kwa sasa inawanafunzi 851, ambapo kati yao Wanaume ni 135 na wananwake 716.
Wanafunzi wanaosoma Shule hiyo, wanafurahia na uwepo wa mazingira mazuri ya kujisomea, vitabu hata walimu na madarasa ya kutosha. Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Nancy Lymo ni ambaye mwanafunzi wa Kidato cha Sita alisema
“ Tunapenda kumshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutuwezesha kupata Shule hii, Tunamshukuru pia Mbunge wetu mama etu Jenista Mhagama kwa kutupambania sisi watoto wa kike, kwa kweli hapa Shuleni tunapata kila kitu ambacho mwanafunzi anahitaji. Mazingira mazuri, vitabu vya kutosha, Majengo mazuri Walimu wapo kwa kweli tunafurahia.
Aidha Mkuu wa Shule naye pia ameshukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwekeza kwenye Elimu kwani vijana wanafurahia kupata elimu katika mazingira mazuri.
Hata Hivyo amemuhakikishia Mhe. Rais na Mbunge kwamba wanafunzi hao watafanya vizuri kwenye matokeo yao ya kidato cha sita na cha nne
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa