• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

BENKI ya Dunia yatoa shilingi milioni 220 kufadhili ujenzi wa miundo mbinu ya afya Wilaya ya Songea

Tarehe ya Kuwekwa: May 17th, 2021

Benki ya Dunia imetoa shilingi milioni 220 kutekeleza Mpango endelevu wa Maji na Usafi wa Mazingira katika Halmashauri ya Wilaya Songea Mkoani Ruvuma.

Kaimu Mganga mkuu wa Halmashauri hiyo Dr Geofrey Kihaule amesema fedha hizo zimetolewa kwa madhumuni ya kutekeleza ujenzi na uboreshaji wa miundo mbinu ya kutolea huduma za afya kwenye Zahanati.

Amesema miundo mbinu inayotakiwa kujengwa na kuboreshwa ni chumba cha kujifungulia akinamama wajawazito, chenye viwango vinavyokubalika Kimataifa,matundu saba ya vyoo ikijuisha choo ya walemavu,kichomea taka,na miundo mbinu ya kutolea huduma ya maji.

Dr kihaule amesema ujenzi wa miundo mbinu ya kutolea huduma za afya kwenye zahanati kutasaidia wananchi hususani akinamama kuwa katika mazingira salama ya kujifungulia na mazingira ya faragha pindi wanapofika katika vituo hivyo.   

Dr kihaule amevitaja Vijiji 10 ambavyo vitanufaika na mradi huo kuwa ni Litowa,Parangu,Lugagara,Peramiho (B),Muungano Zomba,Vijiji ni vingine            ni Mgazini,Kilagano,Ngahokora,Liula na Kikunja.

 Ameongeza kwa kusema muda wa utekelezaji wa mradi ni siku 40 kulingana utaratibu uliopanga wa utekelezaji,katika kufanikisha kazi hiyo vikao kazi baina ya kamati za afya za Vijiji na viongozi wa Serikali za vijiji tayari vimefanyika na ujenzi unatarajia kuanza mara moja kuanzia mwezi Mei  17,2021.

Kwa upande wake Afisa Afya wa Wilaya hiyo na Mratibu wa mradi huo John Kapitingana amesema mradi wa mpango endelevu wa maji na usafi wa mazingira unafadhiri kwa utaratibu wa lipa kulingana na matokeo (EP4R).

“Tushrikiane katika kutoa matokeo chanya ya mradi”,amesisitiza Kapitingana.

Kapitingana ametoa wito kwa viongozi wa vijiji na wananchi kujenga mshikamo na ushirikiano katika kufanikisha ujenzi huo na kutoa matokea chanya ambayo yatasababisha Benki ya Dunia kuendelea kutoa ufadhili kwa zahanati nyingi katika halmashauri.

Baadhi ya viongozi wa kamati ya afya ya Kijiji cha Litowa ambao ni Lukulesi mkinga na abdallah kassimu   wamesema wameupokea mradi na watashirikiana na wananchi kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na unatoa huduma iliyokusudiwa.

Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma inajumla ya Zahanati 24,kituo cha Afya kimoja na Hospitali moja ya Wilaya iliyojengwa Kijiji cha Mpitimbi (B) kata ya Mpitimbi.

Imeandikwa na

Jacquelen Clavery

K/ Afisa Habari Songea DC

17,05,2021

 

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KULA YAMEANZA SONGEA DC

    April 29, 2025
  • MHE . JENISTA MHAGAMA AZINDUA MADARASA 27 NA VYOO MATUNDU 44, SONGEA DC

    March 16, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa