Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya yaSongea Mkoani Ruvuma limepitisha Rasimu ya mpango na matumizi wa bajeti kiasi cha shilingi bilioni 31,695,165,245.85 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Akiwasilisha Rasimu hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi Neema Maghembe amesema chanzo cha fedha hizo kuwa mapato ya ndani,ruzuku toka Serikali kuu na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Bi.Maghenbe amevitaja vipaumbele vya matumizi ya fedha hizo ni ujenzi na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo,matumizi ya mengineyo na mishahara ya watumishi.
Amesema Halmashauri itaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji kwa kutenga maeneo ya uwekezaji,kuimarisha uzalishaji katika sekata ya kilimo hasa katika mazao ya kimkakati ambayo ni korosho,alizeti,soya,mahindi na ufuta kwakuwa kilimo ndio shughuli kuu ya kiuchumi katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Bi.Maghembe ameongeza kwa kusema Rasimu hiyo imezingatia maelekezo yaliyoanishwa kwenye nyaraka muhimu za Serikali ambazo baadhi yake ni dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025,Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020,mapango wa Taifa wa miaka mitano 2021/2022-2025/2026,Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa wakati anafungua bunge la 12 ,na Mpango mkamkati wa wa Halmashauri wa kipindi cha miaka mitano.
Bi.Maghembe ameongeza kwakusema kwa kipindi cha mwaka wa fedha cha 2021/2022 Halmashauri imepata mafanikioa makubwa baadhi ya mafanikio hayo ni ujenzi wa vyumba vya madarasa 65 kupitia mradi wa UVIKO-19 kwa Shule za Sekondari vyumba 46 naShule Shikizi za Msingi vyumba 19,urasimishaji wa viwanja 2500 katika eneo la Peramiho,utatutusi wa migogoro na utoaji wa mikopo kwa wanawake ,vijana na watu wenyeulemavu.
Bi.Maghembe amezitaja baadhi ya changamoto zautekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 uwepo wa miradi viporo,fedha za ufuatiliaji na usimamizi kutokidhi mahitaji,fedha za miradi toka Serikali kuu kutofika kwa wakati au kuto fika kabisa na kuwepo kwa migogoro ya ardhi ya mipaka mashamba na viwanja.
Amesema Halmashauri imaejipanga vizuri kwa kushirikiana na wananchi na wadau wa maeandeleo kuhakikisha changamoto za migogoro zinapatiwa ufumbuzi Pia ufuatiliaji wa fedha za miradi toka Serikali kuu,na kuendelea kuimarisha mbinu na mikakati ya ukusanyaji wa mapato.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa