BARAZA LA Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Kupitia Mkutano wa Baraza maalum la Madiwani wamekutana leo tarehe 30.08.2023 kujadili na kupitisha taarifa ya hesabu za Halmashauri kwa mwaka wa fedha ulioishia 30 Juni, 2023.
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Lundusi-Peramiho.
Katika mkutano huo maalumu Waheshimiwa Madiwani wametoa pongezi kwa Wataalamu kwa kuweza kuandaa taarifa hizo za hesabu kwa umakini na ufanisi mkubwa.
Akisoma taarifa Mweka Hazina wa Halmashauri Bi. Hadija Boffu amesema kwa mujibu wa Sheria za Serikali za mitaa ya Mwaka 1982 kifungu Na. 40 kama kilivyorekebishwa mwaka 2000, Halmashauri nchini zinapaswa kufunga hesabu na kuwasilisha kwa mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) si zaidi ya miezi mitatu baada ya kumaliza mwaka.
Aidha, amesema mfumo wa ufungaji Hesabu Kimataifa ujulikanao kama ( IPSAS International Public Sector Accounting Starndards - Accruals Basis) ndiyo uliotumika katika uandaaji wa Hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Ameongeza kuwa uandaaji wa hesabu kuishia 30 Juni, 2023 umezingatia Sheria za Fedha, Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2011, Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 kama ilivyorekebishwa mwaka 2000, Miongozo inayotolewa na Bodi ya Uhasibu, Sera za Nchi na Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa