Baraza la madiwani limepitisha azimio la kuzuia kupiga chapa ng’ombe kipindi cha masika
Baraza la madiwani limepitisha azimio la kuzuia kupiga chapa ng’ombe kipindi cha masika na badala yake wapigwe chapa kipindi cha kiangazi
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kamati ya uchumi,ujenzi na mazingira Mhe Nestory Mwanja katika kikao cha Baraza la madiwani kilicho fanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Mhe Mwanja amesema ng’ombe wasipigwe chapa kipindi cha masika kwasababu ya kuwanusuru na magomjwa mbalimbali ambayo yanaweza kuwashambulia kutokana na bakteria na hali ya hewa ya kipindi cha masika inayopelekea vidonda vya chapa kutopona haraka na kusababisha adha kwa mfugaji.
Baadhi ya wafugaji wamesema wamefurahishwa na uamuzi wa baraza la madiwani wa kuzuia kupiga ng’ombe chapa wakati wa masika kwasababu ya kulazimika kutoamatunzo ya karibu kwa mifugo hiyo endapo watapata magonjwa yatokanayo na kushambuliwa na bakteria na vidonda kuchelewa kupona kwa haraka
Hata hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Songea mapema mwezi Februari 2017 kupitia vikao ilikataza kuingiza ng’ombe kutoka nje ya Wilaya kwa sababu ya kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambayo inaweza kujitokeza kwakuwa Halmashauri ya wilaya ya Songea ni moja ya Wilaya zinazotegemewa sana katika kilimo hasa kilimo cha mahindi katika Mkoa wa Ruvuma.
JACQUELEN CLAVERY –TEHAMA.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa