BARAZA la madiwani limewafukuza kazi watumishi 4 na kuwarejesha 7 kazini
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma limewafuka kazi watumishi 4 na kuwarejesha kazini watumishi 7
Baraza la madiwa ni limefikia uamuzi huo katika kikao chake cha robo kilicho fanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya songea.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh Rajabu Mtiula amesema baraza la madiwani limewafukuza kazi watumishi 4 na kuwarejesha kazini watumishi wake 7 kati ya hao 6 wanafanyakazi idara ya fedha na mmoja ni Afisa Mtendaji wa Kata.
Amewataja walio fukuzwa kazi baada ya kubainika na makosa ya ubadhirifu wa mali ya umma kwa watendaji,pia maelekezo na maagizo ya Katibu Mkuu Utumushi kwa fundi sanifu mwandamizini Chistophar komba Mtendaji daraja la III,Hashimu Pilli Mtendaji daraja la III,Ally Mtumbuka naye Mtendaji daraja la III, na Zainabu Zuberi aliyekuwa fundi sanifu mwandamizi.
Aidha amewataja waliorudishwa kazi kwa masharti ya kushushwa mshahara kuwa ni Yasini Mohamed,Pendo Kimeme,Cosmas Haule, Aizack Mabula, Adamson Cleophas,wote wa idara ya fedha na Azizi Mbaruku ni Mtendaji wa Kata,aidha Beatice Gauza yeye amerudishwa kazini bila masharti yoyote kwakuwa hakukutwa na kosa lolote.
Ametoa wito kwa wataalamu na madiwani wote kusima ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Songea inayojengwa katika Kata ya Mpitimbi,Kijiji cha Mpitimbi (B)
JACQUELEN CLAVERI /AFISA HABARI SONNGEA DC. moyojacquelen@gmail.com
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa