Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Songea limemchagua tena Diwani wa Kata ya Lilahi Mhe. Simon Boniface Kapinga kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja.
Uchaguzi huo umefanyika kupitia mkutano mkuu wa mwaka wa baraza la madiwani 2022/2023 uliofanyika tarehe 25 Agosti 2023 ikiwa ni utaratibu wa kisheria wa kuchagua makamu mwenyekiti kila mwaka na uundaji wa Kamati mbalimbali za kudumu za Halmashauri.
Aidha, wajumbe waliopiga kura walikuwa 18 hivyo Mheshimiwa Kapinga alishinda kwa kishindo kwa kupata kura zote 18 za ndio.
Kamati zilizoundwa ni kamati ya Maadili, kamati ya kudhibiti UKIMWI, kamati ya Elimu, Afya na Maji, kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, Bodi ya Ajira pamoja na Kamati ya ugawaji Ardhi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Makamu Mwenyekiti na Wenyeviti wa Kamati zilizoundwa wameshukuru wajumbe wa kikao na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha Halmashauri ya Wilaya ya Songea inasonga mbele.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa