Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mh Williamu Lukuvi amepiga marufuku makampuni yayojihusisha na upimaji wa ardhi kuhusika na kazi hiyo.
Waziri Lukuvi ametoa agizo hilo katika hafla fupi ya uzinduzi wa Ofisi ya Ardhi ya Mkoa wa Ruvuma iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma hivi karibuni.
Lukuvi ametoa agizo hilo kufuatia ukiukwaji wa taratibu za upimaji wa ardhi na kusababisha dhuluma na migogoro kwa wananchi.
Amewaagiza wakurugenzi wa Manspa na Wilaya kusimamia kazi za upimaji wa ardhi yote ndani ya mkoa na kupanga matumzi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro kwa wananchi.
"Marufuku kwa mtu yoyote,kampuni au Taasisi kuchukua ardhi ya wananchi bila ya kuwalipa fidia",alisema Lukuvi.
Amewataka watumishi wa idara ya ardhi kuanzia Mkoa na Wilaya kwenda kwa wananchi kutafuta kero za migogoro ya ardhi na kutatua lengo likiwa kumaliza migogoro.
Waziri Lukuvi ametoa siku 90 kwa wadaiwa wa kodi ya ardhi ,kulipa kodi ndani ya kipindi hicho kuanzia tarehe10 /08 /2020 baada ya siku hizo wadaiwa watahesabiwa deni kuanzia siku waliyopata kiwanja mpaka siku ya kuchukua ankara yako.
Kwa upande wake Kamishna msaidizi wa ardhi wa Mkoa wa Ruvuma Bw ILDEFONCE NDEMLA amesema kzinduliwa kwa ofisi za ardhi za Mkoa kutarahisisha utoaji wa huduma ,pamoja kuondoa usumbufu na gharama kwa wananchi ambao walikuwa wakipata wakati wa kwenda kufuata huduma hizo ofisi za kanda Mkoani Mtwara.
Naye Kamishina wa Ardhi Tanzania Nathanieli Mhonge amesema kuanzishwa kwa ofisi za mikoa 26 Nchini ,Wizara inatarajia kuona upangaji na upimaji wa ardhi utaongezeka,kupungua kwa makazi holela,kupunguza migogoro na ukusanyaji wa maduhuri ya serikali unaongezeka.
imeandikwa na Jacquelen Clavery
Afisa habari Songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa