Agizo.
Naibu Waziri wa Afya OR TAMISEM Mh Josephat Kandege (mb) ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea na Mkoa kusimamia kikamilifu ujenzi wa kituo cha Afya Muhukuru na kuhakikisha unakamilika kwa wakati
Ametoa wito huo baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa kituo hicho hivi karibuni.
Mh Kandege amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo hicho unavyoendelea hivyo akatoa agizo kwa uongozi wa Wilaya na Mkoa kuhakikisha ujenzi wa kituo cha Afya na fedha zinasimamiwa vizuri kadiri ya miongozo inavyo ongoza.
Ujenzi wa kituo hicho umegharimu kiasi cha shilingi milioni 99 na umefikia hatua ya msingi katika utekekezaji wake sawa na asilimia 20,ikumbukwe Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi milioni 500 toka OR TAMISEM -AFYA kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu na ujenzi wa majengo matano.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa