Vijana 1681 Wahitimu Mafunzo ya awali ya Kijeshi wa mujibu wa sheria operation Mirerani na 42 wameshindwa kumaliza mafunzo hayo.
Vijana hao wamehitimu mafunzo hayo katika kikosi cha 842 KJ Kikosi cha jeshi –Mlale JKT Septemba 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Christina Mndeme amesema mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana kwa mujibu wa sheria sio adhabu kwa vijana ni sehemu muhimu ya kupata mafunzo ya malezi bora yanayoendana na misingi ya taifa letu pamoja na mafunzo ya kiuzalendo ambayo yanasaidia kuwajenga vijana katika maadili mema.
Mh. Mndeme amewahimiza wazazi na walezi kuwapeleka vijana wao kushiriki mafunzo hayo mara wapatapo fursa hiyo kwakuwa mafunzo hayo yanafaida kwa vijana pamoja na kujenga Afya zao, kuwa wakakamavu na kuwaandaa kuwa viongozi bora kwa siku za baadae.
Aidha amewaasa vijana kutoanzisha migogoro ambayo haina tija kwa taifa, washirikiane katika kufichua maovu kama vile vitendo vya rushwa madawa ya kulevya mimba za utotoni pia kukemea matishio yoyote yauvunjifu wa usalama yanapotaka kutokea na kuwa mfano bora kwa jamii inayowazunguka.
Wahitimu wa mafunzo hayo kupitia risala yao kwa mgeni rasmi wamesema wanaishukuru serikali kwa kurudisha mafunzo ya awali ya kijeshi wa mujibu wa sheria kwakuwa yanatoa fursa kwa vijana kujifunza stadi mbalimbali za maisha, shughuli za ujasiriamali, uzalishajimali na maadili mema katika jamii wanayoishi.
Akizungumzia changamoto zinazokikabili kikosi cha 842KJ Mlale ambazo ni uchakavu wa majengo na miundombinu amesema serikali ya awamu ya tano inaendelea kuzifanyia kazi changamoto hizo na kuzipatia ufumbuzi.
Mafunzo ya awali wa mujibu wa sheria hufanyika kwa muda wa miezi 3 kwa vijana wanaohitimu kidato cha sita na jumla ya Vijana 1681 wamefanikiwa kuhitimu na 42 katiyao wasichana 2 na wavulana 40 wameshindwa kumaliza mafunzo hayo kwa utoro.
JACQUELEN CLAVERY -TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa