MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, anatangaza Ajira kwa watu wenye uzoefu katika ujenzi kutoka sehemu mbalimbali. Kipaumbele kitatolewa kwa mafundi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea wenye sifa.
Nyaraka za maombi zinapatikana kwenye ofisi za wakuu wa shule, fomu za maombi ya kazi (michoro na muainisho wa kazi) zinatolewa kuanzia saa 01:30 asubuhi mpaka saa 09:30 alasiri siku za kazi.
Waombaji wenye nia ya kufanya kazi ya ujenzi wanaweza kupata maelekezo Zaidi katika ofisi ya wakuu wa shule za sekondari.
Taratibu za upatikanaji wa mafundi zitafanyika kwa njia ushindani kwa kuzingatia sheria ya ununuzi wa Umma ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2020.
Siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ni tarehe 17/10/2022 siku ya Jumatatu kabla ya saa 06:30 mchana. Barua za maombi ziwekwe kwenye bahasha na kufungwa vizuri kisha zirejeshwe katika ofisi za wakuu wa shule kabla ya muda ulioainishwa.
Maombi yatakayochelewa, maombi yasiyo kamilika, maombi ambayo hayatakuepo siku ya ufunguzi, hayatapokelewa na kuhusishwa katika zoezi la tathmini ya kumpata fundi.
SIFA ZA MWOMBAJI
S/N
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA MADARASA YATAKAYOJENGWA.
|
1
|
LUPUNGA
|
1
|
2
|
DARAJAMBILI
|
1
|
3
|
MAGAGURA
|
3
|
4
|
MUHUKURU
|
1
|
5
|
KILAGANO
|
2
|
6
|
MPITIMBI
|
2
|
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa